JUAN MATA: NI RASMI, NI MCHEZAJI MANCHESTER UNITED!!
>>MATA: “CHELSEA NI KLABU KUBWA.. LAKINI HUWEZI KUIKATAA NAFASI YA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED!!”
>>KUTAMBULISHWA RASMI JUMATATU JIONI!!
Juan Mata amekamilisha Uhamisho wa Dau la Pauni Milioni 37.1 kutoka Chelsea kwenda Manchester United.
Jana Mata alipimwa Afya yake huko Manchester na kusaini Mkataba unaoaminika kuwa unamalizika Juni 2018.
Mata, Miaka 25, anatarajiwa kucheza
Mechi yake ya kwanza hapo Jumanne Uwanjani Old Trafford na Cardiff City
kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Akiongea baada ya kusaini Mkataba, Mata
alisema: “Umefika wakati wa changamoto nyingine. Nimefurahi mno kuwa
sehemu ya awamu nyingine ya historia ya Klabu hii.”
Aliongeza: “Chelsea ni Klabu kubwa na
nia Marafiki wengi kule lakini huwezi kuikataa nafasi ya kujiunga na
Manchester United. Ninatarajia kumsaidia Meneja na Timu kupata mafanikio
zaidi katika Miaka ijayo!”
Mata anakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa
na Meneja David Moyes baada kumsaini Marouane Fellaini kutoka Everton
Mwezi Septemba kwa Dau la Pauni Milioni 27.5.
Pia, kwa kumsaini Mata, Man United
imevunja Rekodi yao ya kusaini Mchezaji kwa Bei ya juu ambayo iliwekwa
Mwaka 2008 walipomsaini Dimitar Berbatov kwa Pauni Milioni 30.
Mata atatambulishwa rasmi kama Mchezaji mpya wa Man United Jumatatu Saa 10 na Nusu Jioni, Saa za Tanzania.
+++++++++++++++++++++++++++
WASIFU:
Jina: Juan Manuel Mata García
Kuzaliwa: 28 Aprili 1988 (Miaka 25)
Namba ya Jezi: 10
Timu za Vijana
1998–2003 Real Oviedo
2003–2006 Real Madrid
Timu za Kwanza
[Magoli kweye Ligi tu]
2006–2007 Real Madrid B Mechi 39 Goli 10
2007–2011 Valencia Mechi 129 Goli 33
2011– Chelsea Mechi 82 Goli 18
Timu ya Taifa
2004 Spain U16 Mechi 3 Goli 2
2004 Spain U17 Mechi 2 Goli 1
2006–2007 Spain U19 Mechi 13 Goli 12
2007 Spain U20 Mechi 5 Goli 3
2007–2011 Spain U21 Mechi 19 Goli 5
2012 Spain U23 Mechi 4
2009– Spain Mechi 32 Goli 9