SERIE A: BUFFON NYEKUNDU, JUVE SARE!
>>LEO AS ROMA, INTER MILAN, AC MILAN ZOTE DIMBANI!
Lile wimbi la ushindi la Mechi 12 mfululizo kwa Juventus Jana limefika tamati baada kubahatikakutoka Sare ya Bao 1-1 na Lazio huku wakicheza Mtu 10 baada Kipa wao Veterani, Gianluigi Buffon, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Buffon, Miaka 35, alipewa Kadi Nyekundu
katika Dakika ya 24 kwa kumchezea rafu Miroslav Klose na ikatolewa
Penati iliyofungwa na Antonio Candreva.
Lakini Juve walinusurika kipigo baada
Fernando Llorente kusawazisha kwa kichwa katika Dakika ya 60 na kuwapa
Pointi 1 ambayo imewabakisha kileleni mwa Serie A wakiwa Pointi 14 mbele
ya AS Roma ambao wamecheza Mechi 1 pungufu.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Juventus |
21 |
18 |
2 |
1 |
51 |
15 |
36 |
56 |
2 |
AS Roma |
20 |
14 |
5 |
1 |
42 |
10 |
32 |
47 |
3 |
Napoli |
21 |
13 |
5 |
3 |
44 |
23 |
21 |
44 |
4 |
Fiorentina |
20 |
12 |
4 |
4 |
37 |
20 |
17 |
40 |
5 |
Inter Milan |
20 |
8 |
8 |
4 |
38 |
24 |
14 |
32 |
6 |
Hellas Verona |
20 |
10 |
2 |
8 |
34 |
31 |
3 |
32 |
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi nyingine ya Serie A
iliyochezwa Jana, Bao la Raul Albiol la Dakika ya 88 liliwaokoa Napoli
na kutoka Sare ya 1-1 na Chievo Verona ambao walifunga Bao lao Dakika ya
18 kupitia Gennaro Sardo.
RATIBA:
Jumapili Januari 26
[Saa za Bongo]
14:30 Hellas Verona FC v AS Roma
17:00 Inter Milan v Calcio Catania
17:00 Parma FC v Udinese Calcio
17:00 Torino FC v Atalanta BC
17:00 UC Sampdoria v Bologna FC
17:00 AS Livorno Calcio v US Sassuolo Calcio
17:00 Cagliari Calcio v AC Milan
22:45 ACF Fiorentina v Genoa CFC