Header Ads

LIGI KUU ENGLAND-JUMATANO: WHITE HART LANE SPURS v CITY

STAMFORD BRIDGE: CHELSEA v WEST HAM!!
PATA TATHMINI/VIKOSI MECHI ZOTE ZA JUMATANO:
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City
++++++++++++++++++++++++++
ASTON VILLA v WEST BROM
BPL2013LOGOKwenye Mechi yao ya kwanza Mwezi Novemba, West Brom walitangulia Bao 2-0 hadi Mapumziko kwa Bao mbili za Shane Long, ambae Juzi amehamia Hull, lakini Villa walizinduka Kipindi cha Pili na kutoka Sare ya Bao 2-2 kwa Bao za Karim El Ahmadi na Ashley Westwood.
Mbali ya Long kuihama West Brom, pia sasa wana Meneja mpya, Pepe Mel, kutoka Spain, na walitoka Droo ya 1-1 na Everton katika Mechi yake ya kwanza Wiki iliyopita huku Villa nao wakitoka Droo ya 2-2 na Klabu nyingine ya Merseyside, Liverpool, katika Mechi iliyopita.
Timu hizi, ambazo zote zinatoka maeneo ya Midlands huko England, zina upinzani wa Jadi na katika Mechi zao 15 zilizopita Matokeo huwa ni Sare au moja hushinda 2-1 lakini kwa ujumla Villa wanaongoza kwa kushinda Mechi nyingi kati yao.
Kila Timu inatarajiwa kuwa na Kikosi kamili isipokuwa West Brom ambao watamkosa Stephane Sessegnon mwenye tatizo la Nyonga.
VIKOSI VITATOKANA NA:
Aston Villa : Guzan, Steer, Baker, Bennett, Bertrand, Clark, Lowton, Luna, Vlaar, Albrighton, Bacuna, Delph, El Ahmadi, Gardner, Herd, Johnson, Sylla, Tonev, Westwood, Agbonlahor, Benteke, Bowery, Helenius, Holt, Weimann.
West Brom: Daniels, Foster, Myhill, Dawson, Jones, Lugano, McAuley, Olsson, Popov, Reid, Ridgewell, Amalfitano, Brunt, Dorrans, Gera, Morrison, Mulumbu, Thorne, Yacob, Anelka, Anichebe, Berahino, Rosenberg, Sinclair, Vydra.
Refa: Mark Clattenburg.
CHELSEA v WEST HAM
ETOO_IN_CHELSEA2Chelsea wanajikita kwenye Mechi hii Uwanjani kwao wakitoka kwenye ushindi wa Mechi 5 mfululizo za Ligi na wanakutana na West Ham ambayo imeshinda Mechi 1 tu kati ya 9 walizocheza mwisho kwenye Mashindano yote.
West Ham hawajashinda Stamford Bridge tangu 2002 wakipoteza Mechi 7 kati ya 8 walizocheza mwisho hapo na walipigwa 3-0 na Chelsea Mwezi Novemba walipocheza Upton Park kwenye Mechi ya Ligi.
Chelsea itamkosa Fernando Torres, mwenye maumivu ya Goti, lakini Mchezaji wao mpya kutoka Benfica, Nemanja Matic, huenda akaanza Mechi hii, baada kuingizwa kutoka Benchi kucheza Mechi iliyopita ya FA CUP.
Pia, huenda mpya mwingine wa Chelsea kutoka FC Basel ya Uswisi, Chipukizi wa Misri, Mohamed Salah, akachezeshwa kwenye Mechi hii.
West Ham, chini ya Meneja Sam Allardyce, inacho Kikosi chao kamili cha kuchagua Timu yao
VIKOSI VITATOKANA NA:
Chelsea : Blackman, Cech, Hilario, Schwarzer, Ake, Azpilicueta, Cahill, Cole, Ivanovic, Kalas, Luiz, Terry, Hazard, Lampard, Matic, Mikel, Oscar, Ramires, Salah, Willian, Ba, Eto’o, Schurrle.
West Ham: Adrian, Henderson, Jaaskelainen, Collins, Demel, Johnson, McCartney, O'Brien, Potts, Rat, Tomkins, Collison, Diame, Diarra, Downing, Jarvis, Morrison, Noble, Nolan, Nocerino, Taylor, Carroll, C Cole, Lee, Maiga, Petric, Vaz Te, Borriello.
Refa: Neil Swarbrick.
SUNDERLAND v STOKE CITY
Stoke City wanasafiri kwenda kucheza na Sunderland wakisaka ushindi wao wa kwanza ndani ya Stadium of Light tangu Aprili 1994 na baada hapo kutoshinda katika Mechi 11.
Sunderland, chini ya Meneja mpya Gus Poyet, wamefungwa Mechi 1 tu ya Ligi kati ya 7 na wametinga Fainali ya Capital One Cup na Raundi ya 5 ya FA CUP.
Stoke wana matatizo kwenye Mechi zao za Ugenini na watajaribu kukwepa kumaliza Mechi 10 mfululizo za Ligi bila ushindi na kipigo cha 5 mfululizo katika Mashindano yote.
Lakini katika Mechi zao 3 zilizopita , Stoke City hawajafungwa na Sunderland.
Stoke wameimarika kwa Kipa wao Nambari Wani, Asmir Begovic, kurudi tena baada kupona Kidole alichovunjika na kucheza vyema sana alipozuia Bao nyingi walipofungwa 1-0 na Chelsea Juzi kwenye FA CUP.
Pia huenda Stoke wakamtumia Mchezaji mpya, Peter Odemwingie, abae amehamia hapo kutoka Cardiff baada kubadilishana na Kenwyne Jones alietoka Stoke kwenda Cardiff.
VIKOSI VITATOKANA NA:
Sunderland: Mannone, Pickford, Alonso, Bardsley, Brown, Celustka, Diakite, Dossena, O'Shea, Roberge, Ba, Cabral, Cattermole, Colback, Gardner, Giaccherini, Johnson, Ki, Larsson, Mavrias, Altidore, Borini, Fletcher, Moberg-Karlsson, Wickham.
Stoke City: Begovic, Butland, Sorensen, Cameron, Muniesa, Pieters, Shawcross, Shotton, Wilson, Adam, Assaidi, Edu, Ireland, N’Zonzi, Palacios, Whelan, Arnautovic, Crouch, Jones, Walters, Guidetti.
Referee: Robert Madley
TOTTENHAM v MAN CITY
Ingawa waliichapa Tottenham Hotspur 6-0 Msimu huu huko Etihad Stadium, Meneja wa Man CityADEBAYOR-SPURS Manuel Pellegrini anategemea upinzani mkali watakapotua White Hart Lane Jumatano.
Tangu wapfungwe Bao hizo 6-0, Meneja wa Spurs, Andre Villas-Boas alitimuliwa na kubadilishwa na Tim Sherwood na wameshinda Mechi za Ligi huku Straika wao Emmanuel Adebayor akirudishwa tena Timu ya Kwanza na kuongoza katika ufungaji kwa kupachika Bao 6 katika Mechi 8.
Msimu uliopita, Spurs waliichapa Man City Bao 3-1 Uwanjani White Hart Lane.
Spurs wanaweza kuwa nao tena Majeruhi wao Paulinho, Andros Townsend, Jan Vertonghen na Sandro ingawa ipo hatihati kwa Younes Kaboul.
Man City nao wanatarajiwa kuwa nae David Silva ambae amepona tatizo la Musuli za Pajani baada kukosa Mechi kadhaa.
VIKOSI VITATOKANA NA:
Spurs: Friedel, Gomes, Lloris, Chiriches, Dawson, Naughton, Rose, Vertonghen, Walker, Capoue, Chadli, Dembele, Eriksen, Holtby, Lamela, Lennon, Paulinho, Sigurdsson, Townsend, Adebayor, Defoe, Soldado.
Manchester City: Hart, Pantilimon, Boyata, Clichy, Demichelis, Kolarov, Kompany, Lescott, Nastasic, Richards, Zabaleta, Garcia, Fernandinho, Milner, Nasri, Navas, Rodwell, Silva, Toure, Aguero, Dzeko, Jovetic, Negredo
Refa: Andre Marriner
MSIMAMO:
[Kabla ya Mechi za Jumanne Januari 28]
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
22
24
51
2
Man City
22
38
50
3
Chelsea
22
23
49
4
Liverpool
22
25
43
5
Tottenham
22
3
43
6
Everton
22
15
42
7
Man Unit3d
22
9
37
8
Newcastle
22
4
36
9
Southampton
22
4
31
10
Aston Villa
22
-7
24
11
Hull
22
-6
23
12
Norwich
22
-17
23
13
West Brom
22
-5
22
14
Stoke
22
-14
22
15
Swansea
22
-6
21
16
Crystal Palace
22
-17
20
17
Fulham
22
-26
19
18
West Ham
22
-11
18
19
Sunderland
22
-15
18
20
Cardiff
22
-21
18
Powered by Blogger.