SMZ YASHAURIWA KUIMARISHA HALI YA USALAMA WA ENEO LA NYARAKA
Na Miza Kona -Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi imeshauriwa kuimarisha hali ya usalama wa eneo la Nyaraka
kwa kuweka kamera za kuangaza usalama kwa ukaribu CCTV ili kuepusha wizi
usitokee katika Idara hiyo.
Akiwasilisha
Muhtasari wa Ripoti ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza La
Wawakilishi kwa mwaka wa Fedha 2013/2014 Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ussi
Jecha Simai amesema kuwekwa vyombo vya usalama katika idara hiyo
kutasaidia kuepusha kuibiwa kwa nyaraka za Taifa na kuipatia hasara
nchi.
Aidha
amesema Kamati imesikitishwa na na taarifa za wizi wa nyaraka muhimu
uliotokea katika Idara na kusisitiza kuwekwa kwa vyombo vya CCTV ili
kuweza kubaini wizi huo unapofanyika. Pia
Kamati hiyo wameomba serikali kupitia vyombo vyake usalama kufanya
uchuzi wa tukio hilo kwa kila aliyehusika na wizi wa nyaraka kuchukuliwa
hatua za kisheria.
Hata
hivyo Kamati hiyo imeitaka serkali kuandaa mpango wa kuzifanyia ukaguzi
Nyaraka zote zikiwemo Ofisi ya Vizazi na Vifo pamoja na Wakfu na baada
ya muda na ripoti yake ipelekwe katika Baraza ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Wizara.
“Hivi
sasa Idara ya Nyaraka imefanywa kama vile ni eneo la kuhifadhia vitu
vya kale visivyohitajika tena, eneo lenyewe lipo katika hali hatarishi
kiusalama, jengo finyu,halitoshelezi kuhifadhi kwa ufanisi nyaraka
nyingi zilizomo”,alieleza.
Aidha
alifahamisha kuwa ustawi wa kiafya kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo upo
katika hali ya hatari kutokana na mazingiramagumu wanayofanyia kazi
kwa kukosa vifaa muhimu ikiwemo ukosefu wa vipoza hewa katika vyumba
vya kuhifadhia Nyaraka.
Akichangia
Ripoti ya Kamati hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame mshimba
Mbarouk amesema wizi wa nyaraka umesababishwa kudharauliwa na
kutothaminiwa kwa nyaraka za asili pamoja na ukosefu wa vifaa muhimu wa
kuchunguza na kubaini wizi unafanyika hivyo serikali ichukuwe hatua za
kisheria kwa yoyote atakaehusika na wizi huo.
Aidha
ameiomba serikali kuanzisha Mahakama za wawekezaji ambazo zitaweza
kutekeleza kazi zake ili kuepusha unyang’anyi wa ardhi pale wanapokuja
kuwekeza na kupata haki zinazostahiki.