Wagombea nao wakijifariji kwa makofi ya wajumbe
KAIMU
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga amewasihi
wajumbe wa mkutano huo kumchangua mgombea anayoonekana kukubalika kwa asilimia
60 kwa wapiga kura.
"Falsafa
ya chama kwanza, mtu baadaye lazima tuipime vizuri, tunahitaji ushindi na ili
tupate ushindi lazima tuangalie wananchi wanataka nini," alisema.
Akifungua
mkutano huo, Mtenga aliwataka wagombea ndani ya chama hicho wawe na utamaduni
wa kukubali matokeo kwa afya ya chama.
Alisema
wagombea wote tisa waliojitokeza katika kura hizo za maoni wana sifa za kuwa
wabunge na akawataka wajumbe kutumia busara zaidi wakati wakifanya uamuzi.
Alisema
mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho umecchukua siku mbili hali
itakayosaidia kukinusuru chama na mipasuko.
“Tulikuwa
na kawaida ya kufanya kura za maoni kwa zaidi ya mwezi mmoja; hali hiyo ilikuwa
ikiwaacha wagombea katika majeraha
makubwa ya matumizi ya fedha,” alisema.
Alisema
majeraha hayo yamekuwa yakichangia hasira kwa wagombea walioshindwa ambao
badala ya kukisaidia chama kipate ushindi, hufurahia kinapopoteza nafasi.
Alisema
kwa mtaji walionao, CCM wana hakika na ushindi wa kishindo katika jimbo hilo
lililoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
Waliojitokeza
kupitia katika chama hicho ni pamoja na Jackson Kiswaga, Hafsa Mtasiwa, Godfrey
Mgimwa.
Wengine ni Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kisaba, Msafiri
Pagamila na Thomas Mwakoka.
|