MGOMO WA WAFANYABISHARA IRINGA WAENDELEA, WATOA MASHARTI YA KUFUNGUA MADUKA YAO
sehemu ya wafanyabishara hao |
Mwenyekiti wa TCCIA, Mwakabungu akifafanua baadhi ya mambo |
WAFANYABIASHARA
walioko katika mgomo wa kutumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD) wa mjini
Iringa wamekubaliana kuendelea na mgomo wao mpaka pale serikali itakaposikiliza
kilio chao.
Mapema
hii leo wafanyabiashara hao walikubaliana kufunga maduka yao wakipinga matumizi
yam shine hizo zinazouzwa kwa kati y ash 600,000 na sh 800,000.
Katika
kikao chao walichofanya kati ya saa nane mchana hadi saa 11 jioni ya leo,
wafanyabiashara hao wamesema ni bora wapate hasara katika biashara zao kuliko
kuendelea kukubalina na kila kitu kinachoamuliwa na serikali.
Kikao
hicho kilifanywa kwa urataibu wa Chemba ya Biashara, wenye Viwanda na Kilimo
(TCCIA) Mkoa wa Iringa.
Hatufungui
maduka mpaka tutakapokutana na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani
hapa, wabunge wote wa Iringa Mjini, Mkurugenzi na Madiwania wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, alisema mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina
la Lusajo.
Lusajo
alisema mshine hizo zimegeuka kero kwa wafanyabishara wengi na akashangaa
sheria ya kukwepa kutoa risiti kwa wateja ikiwalazimu kulipa faini ya Sh
Milioni 3.
“Yaani
mfanyabiashara anayeshindwa kutoa risiti kwa kuuza pakti ya sigara, peni au
karatasi analipa faini sawa na anayekwepa kutoa risiti kwa bidhaa zinazojaa
kontena nzima,” alisema Mzee Kaundama.
Alisema
sheria hiyo haiwatendei haki wafanyabishara wengi na imekuwa ikitengeneza
mazingira ya rushwa kwa maafisa wa TRA.
Alisema
inawezekanaje kwa mfanyabiashara mwenye mtaji wa Sh Milioni moja akalipa kodi
ya mapato asilimia 30, Ongezeko la Kodi ya Thamani asilimia 18 na akafanya
marejesho kwa riba ya asilimia 25 ya mkopo aliochukua kutoka katika taasisi za
fedha.
“Hakuna
mfanyabishara anayekataa kulipa kodi, lakini kwa mazingira hayo mfanyabishara
huyo anayehitaji mazingira rafiki na serikali yake atabakiwa na nini baada ya
kolipa kodi hizo, kodi ya pango na gharama zingine za uendeshaji?” alisema.
Mwenyekiti
wa TCCIA, Lucas Mwakabungu alisema chemba yao iko pamoja na wafanyabishara hao
na akaishangaa serikali kwa kuwa na lundo la kodi kwa wafanyabishara wake.
“Tuna
kodi zaidi ya 24 katika nchi hii, tofauti na wenzetu wa Rwanda wenye kodi
zisizozidi 12,” alisema.
Hata
hivyo alisema shida ya nchi hii sio serikali, ni tabia ta watendaji wabovu
wanaopaswa kuwajibishwa lakini wanaendelea kulindwa.
“Yalipoanzishwa
matumizi ya mashine hizo hakukuwa na maoni kutoka kwa wadau, leo maamuzi
yaliyofanywa na wachache yanawathiri wao, serikali na wananchi wanaowatumikia,”
alisema.
Alisema
serikali inatakiwa kuwafukuza kazi watu waliohusika na mapendekezo ya
uanzishaji wa matumizi ya mashine hizo kwakuwa mchakato wake haukufuata
taratibu shirikishi.