MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM APANDISHWA KIZIMBANI
Madabiba |
OFISA Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Pharmaceutical
Industries (TPI) Ltd, Ramadhani Madabida amefikishwa mahakamani akidaiwa
kusamba dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV).
Madabida na wenzake watano, wakiwemo watumishi wa Boahari
Kuu ya Dawa (MSD), walipandishwa kizzimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu
Dar es Salaam.
Kwa kusambaza dawa hizo feki, Madabida ambaye pia ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na wenzake watano wanadaiwa
kuisababishia serikali hasara ya Sh Milioni 148.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo namba tano ya uhujumu
uchumi ni wafanyakazi wa TPI, Mkurugenzi wa Uendeshaji Seif Shamte, Meneja
Masoko Simon Msofe na Mhasibu Msaidizi Fatma Shango.
Watumishi wa MSD ni Meneja Udhibiti Ubora, Sadiki Materu na Ofisa Udhibiti Ubora, Evans Mwemezi.