ALAN PARDEW: ‘MENEJA WA NDONGA’ KUMVAA PILATO FA!!
MENEJA
wa Newcastle, Alan Pardew, amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka
England, kwa kumtwanga Kichwa Mchezaji wa Hull City, David Meyler.
Pardew, Miaka 52, alitolewa nje na Refa
kwenye Kipindi cha Pili cha Mechi ya Ligi Kuu England kati ya Newcastle
na Hull City ambapo, wakati huo, Newcastle walikuwa mbele kwa Bao 3-1 na
Pardew kuvaana na Meyler baada Mchezaji huyo kumsukuma wakati Mpira
ulitoka nje na uwe wa kurushwa.
Mara baada ya Mechi hiyo, Pardew aliomba radhi na Klau yake kumtwanga Faini ya £100,000 na kumpa Onyo rasmi.
Pardew amepewa hadi Machi 6 kutoa utetezi wake.
Ishu hii ya Pardew imeibua hisia kali
toka kwa Wachambuzi huko England ambao wanadai hii ni kali kupita ile ya
Paul Ince kumsukuma mmoja wa Waamuzi na kufungiwa Mechi 5.
Baadhi ya Wachambuzi wamedai Pardew afungiwe si chini ya Mechi 10 na asiruhusiwe ndani ya Uwanja kwa Kipindi hicho.
Nao Polisi wa eneo la Humberside wamedai
hamna hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi ya Pardew kwa vile kulikuwa
hamna malalamiko yeyote toka kwa Mchezaji husika na Klabu ya Hull City.
Pardew, ambae alikuwa Meneja wa Klabu za
Reading, West Ham, Charlton na Southampton, alijiunga na Newcastle
Desemba 2010 na hadi sasa ameshinda Mechi 59 kati ya 152 kwenye Klabu
hiyo.