KIMATAIFA KIRAFIKI: DIEGO COSTA KUICHEZEA SPAIN KWA MARA YA KWANZA!
>BRAZIL WAKO BONDENI!
JUMATANO
Usiku Mechi za Kimataifa za Kirafiki zitarindima Viwanja mbalimbali
Duniani na huko Madrid, Mabingwa wa Dunia, Spain, watatinga Uwanjani
kujipima na Italy huku macho ya wengi yakimkodolea Straika wa Atletico
Madrid, Diego Costa, akichezea Mechi ya kwanza Nchi yake mpya Spain.
Diego Costa ni Mzaliwa wa Brazil na
ameshaichezea Nchi hiyo Mechi mbili za Kirafiki lakini Mwaka Jana
aliamua kuikana na kuamua kuiwakilisha Spain.
Jumatano Spain watashuka Uwanja wa Vicente Calderon kucheza na Italy.
Akimuongelea Diego Costa, ambae anazo
Goli 21 kwenye La Liga akiwa na Timu yake Atletico Madrid, Kocha wa
Spain Vicente Del Bosque, amesema: “Yeye ni ishu ya kustaajabisha,
hajaitwa Timu ya Taifa kwa sababu kazaliwa Brazil. Lakini tumemwita kwa
sababu ya mafanikio yake na Klabu yake na tunaamini atatusaidia. Ndio
sababu tumemwita na hatuna sababu nyingine.”
Huku akaitarajiwa kutangaza Kikosi chake
kitakachokwenda kwenye Kombe la Dunia huko Brazil hapo Mei 25, Vicente
Del Bosque anatarajiwa kuwapima Wachezaji kadhaa.
Nao Italy, ambao wametoka Sare Mechi zao
mbili zilizopita za kujipima dhidi ya Germany na Nigeria, baada ya
Mechi hii na Spain, watacheza Mechi nyingine mbili na Republic of
Ireland na Luxembourg kabla ya Fainali za Kombe la Dunia ambako
watafungua dimba na England huko Manaus, Brazil Juni 14.
Kwenye Mechi hii na Spain, Italy
itawakosa Danielle De Rossi, Kiungo wa AS Roma ambae ameachwa baada
kumtandika ngumi Mauro Icardi walipotoka 0-0 na Inter Milan Jumamosi
iliyopita na pia Mario Balotelli ambae ameumia Bega.
Spain wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kuifunga Equitorial Guinea 2-1 na kupigwa 1-0 na South Africa Mwezi Novemba.
SOUTH AFRICA v BRAZIL
Kikosi cha Brazil, chini ya Kocha Luiz
Felipe Scolari, kipo Nchini South Africa kupambana na Timu ya Taifa ya
Nchi hiyo, Bafana Bafana.
Brazil wanatinga kwenye Mchi hii wakiwa
wameshinda Mechi zao 6 za Kirafiki zilizopita na watacheza Mechi
nyingine 3 kabla ya Fainali za Kombe la Dunia.
South Africa itaingia kwenye Mechi hii
ikiwa na morali kubwa baada ya kuwatungua Mabingwa wa Dunia, Spain, Bao
1-0 Mwezi Novemba kwenye Mechi iliyochezwa Soccer City, Johannesburg.
Brazil watafungua Fainali za Kombe la Dunia hapo Juni 12 kwa kucheza na Croatia.
MECHI za KIMATAIFA KIRAFIKI
RATIBA
[Muda ukitajwa ni Bongo Taimu]
Jumatano Machi 5
Pakistan Vs Afghanistan
Honduras Vs Venezuela
Malawi Vs Zimbabwe
Morocco Vs Gabon
Mozambique Vs Angola
Senegal Vs Mali
Panama Vs Peru
Namibia Vs Tanzania
Mauritania Vs Niger
Zambia Vs Uganda
Congo Vs Libya
Grenada Vs Jamaica
12:00 Australia Vs Ecuador
13:40 Japan Vs New Zealand
15:30 India Vs Bangladesh
16:30 Burundi Vs Rwanda
20:00 Russia Vs Armenia
20:00 Georgia Vs Liechtenstein
20:00 Iran Vs Guinea
21:00 Lithuania Vs Kazakstan
21:00 Azerbaijan Vs Philippines
20:00 Hungary Vs Finland
20:00 Greece Vs South Korea
20:00 Albania Vs Malta
20:00 Algeria Vs Slovenia
20:00 South Africa Vs Brazil
20:00 Montenegro Vs Ghana
20:30 Israel Vs Slovakia
20:30 Bosnia Vs Egypt
20:30 Czech Republic Vs Norway
21:00 Cyprus Vs Northern Ireland
21:00 Macedonia Vs Latvia
21:00 Andorra Vs Moldova
21:00 Colombia Vs Tunisia
21:30 Luxembourg Vs Cape Verde
21:30 Turkey Vs Sweden
22:00 Romania Vs Argentina
22:00 Ukraine Vs United States
22:00 Gibraltar Vs Estonia
22:30 Austria Vs Uruguay
22:30 Switzerland Vs Croatia
22:45 Poland Vs Scotland
22:45 Germany Vs Chile
22:45 Belgium Vs Ivory Coast
22:45 Wales Vs Iceland
22:45 Ireland Vs Serbia
23:00 France Vs Netherlands
23:00 England Vs Denmark
22:45 Portugal Vs Cameroon
23:00 Spain Vs Italy
23:59 Saint Lucia Vs Jamaica
Alhamisi Machi 6
1:30 Mexico Vs Nigeria
2:00 Costa Rica Vs Paraguay