Carles Puyol kuhama Barcelona
Carles Puyol.
Nahodha wa klabu ya Barcelona Carles Puyol ametangaza atawahama mabingwa hao wa Hispania mwishoni mwa msimu huu.
Puyol mwenye umri wa miaka 35 aliibukia kutoka vikosi vya vijana wa Barcelona na kujiunga na kikosi kikuu mwaka 1999, amewachezea mabingwa watetezi wa La Liga takriban mara 400.
Ameshinda vikombe sita vya ubingwa wa Ligi,vikombe vitatu vya klabu bingwa ya Ulaya,vikombe viwili vya shirikisho la kandanda la Uhispania pamoja na vikombe vya super cup vya klabu za ulaya na Uhispania, pia amekua mchezaj muhimu katika nyanja ya kimataifa akiisaidia Hispania kunyakua ubingwa wa bara la Ulaya mwaka 2008 na kombe la dunia miaka miwili badae.
Hata hivyo amekua akisumbuliwa na magoti katika miaka ya hivi karibuni na hakuweza kushiriki katika michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012, msimu huu ameichezea Barcelona mara 12 tu.
Puyol, ambae ameiwakilisha Hispania mara 100,alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Uruguay, Februari 2013, amesema angependa kupumzika baada ya kuondoka Barcelona. "sijui ntakachofanya baada ya Juni 30 lakini nina hakika nitapumzika" akaongeza. "nitaitisha mkutano na waandishi habari mwishoni mwa msimu huu ili niwaage baada ya kuichezea klabu hii kwa muda wa miaka 19 ," alisema Puyol.
Chanzo,bbcswahili (R.M)