WAVAMIZI NA WAARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI WATAKIONA CHA MOTO.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw Nyirembe Munasa Amesema serikali itwachukulia hatua kali za
kisheria watu wanaovamia na kuaribu vyanzo vya maji ili kukomesha tabi hiyo
pamoja na kuboresha vyanzo hvyo.
Ameyasema hayo wakati akizingua miradi ya maji ya visima
viwili pamoja na kujengea usio kulinda vyanzo hivyo katika wiki ya maji na nishati Mkoani Arusha katika Wilaya ya
Arumeru Kijiji cha Loruvani yaliyosimamimiwa na mamlaka ya Maji Arusha AUWSA ambapo
amewataka wavamizi kuacha tabia hiyo mara moja
Bw Nyirembe amesema maji ni uhai hivyo kuahidi kuwachukulia
hatua kali za kisheria watu wote ambao watahusika katika kuhujumu miradi hiyo
ya maji kwakuwa sheria zipo wazi kwa yeyote atakaye kiuka taratibu na sheria za
kulinda vyanzo hivyo muhimu vya maji.
Pamoja na hayo amesema serikali peke yake haiwezi kupambana
na matukio hayo hivyo kuwataka wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali
kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha wanatatua tatizo la uharibifu wa vyanzo
vya maji pamoja na kutatua tatizo la maji.
Hata hivyo Mkurugenzi
mtendaji wa mamlaka hayo Mkoa wa Arusha Bw Fabia Maganga amesema wanakabiliwa
na changamoto mbalimbali kama vile utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na
ongezeko la Watumia wa huduma hiyo hivyo
kusababisha kuwapo na uhaba mkubwa wa maji safi na salama.
Kauli mbiu katika wiki ya Maji na Nishati ni Uhakika wa maji na Nishati kwakuwa
mategemezi ya maji katika sekta ya nishati ni makubwa hivyo kuwataka wananchi
kuona ulazima wa kutunza na kulinda vyanzo vya maji