Header Ads

UGONJWA HATARI WATINGA NCHINI, UNAAMBUKIZWA NA MBU, DAMU HUTOKA KWENYE MACHO


Dk Rashid

Na Gordon Kalulunga wa Kalulunga Blog

UGONJWA wa ajabu, umeibuka nchini Tanzania, ambao dalili zake zinafanana na ugonjwa wa Malaria. Imebainika.

DENGE. Ndiyo jina la ugonjwa huo, ambao huambukizwa na mbu mwenye wa mabaka yenye mng'aro, dalili zake huanza kuonekana baada ya siku tatu mpaka 14 baada ya mwanadamu kung'atwa na mbu huyo.

Vimelea vya ugonjwa huo au virusi hivyo, tayari vimeonekana kwa wagonjwa 70 Jijini Dar es Salaam na tayari mmoja amekwisha fariki.

Dalili zake ni mtu kujisikia homa kali, viongo vyote vya mwili kuuma kisha kuanza kuanza kutokwa na damu sehemu za fizi, macho na eneo la haja kubwa.

Mtu akiona dalili hizo ni vema akawahi hospitali ingawa bado haijajulikana kinga wala tiba yake, bali kinachofanyika ni kumuongezea mgonjwa maji au damu ili kuokoa maisha yake.

Mbu hao ameelezwa kuwa wanazaliana kwenye maeneo yenye majimaji, hivyo wananchi wanatakiwa kuweka mazingira safi na kavu ili Mbu hao wa ajabu wasiweze kuzaliana.

Mbali na kufanya hivyo, wananchi wanatakiwa kuvaa nguo ndefu yakiwemo mashati ya mikono mirefu ili kumzuia Mbu huyo kutowaambukiza virisi hivyo hatari.

Ugonjwa huo, unaelezwa kuingia nchini tangu mwaka 2010. Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Seif Suleiman Rashid, amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo hasa Jijini Dar es Salaa.
Powered by Blogger.