MKUU WA MKOA WA MARA AFARIKI DUNIA
RC Mara John Tupa |
Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa amefariki dunia
majira ya saa 5 asubuhi ya leo katika Hospitali ya wilaya ya Tarime, baada ya
kuanguka ghafla na kutokwa na povu wakati akitoka nje ya ofisi ya Mkuu wa
Wilaya (DC) Tarime.
Baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa huyo alikimbizwa hospitalini na akafariki dunia muda mfupi wakati timu ya madaktari wa hospitali hiyo ikijiendelea na harakati za kunusuru maisha yake.
Baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa huyo alikimbizwa hospitalini na akafariki dunia muda mfupi wakati timu ya madaktari wa hospitali hiyo ikijiendelea na harakati za kunusuru maisha yake.
Mmoja wa watu waliokuwa jirani na
kiongozi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita alisema “nina mfahamu
marehemu na naweza kusema alikuwa ni mwalimu wangu bingwa wakati nikiwa Dodoma.”
Huku akitokwa na machozi kwa
mbali, Guninita alisema ameguswa na kifo cha kiongozi huyo aliyekuwa
akitegemewa na familia yake na maendeleo ya Taifa.
Mungu ametoa, Mungu ametwa, jina
la Mungu lihimidiwe