ARSENAL KUSAJILI BONGE LA BEKI LA REAL, WENGER PIA APANGA KUMREJESHA FABREGAS KLABU ya Arsenal intake kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad mwenye thamani ya Pauni Milioni 18, Antoine Griezmann - wakati pia inafikiria kumrejesha Nahodha wake wa zamani, Cesc Fabregas. Griezmann, mwenye umri wa miaka 23, amewavutia was aka vipaji wengi The Gunners na klabu imedhamiria kumsajili Mfaransa huyo, ambaye yumo kwenye kikosi cha kocha Didier Deschamps cha Kombe la Dunia. Akizungumza Machi mwaka huu, kocha Arsene Wenger alisema: "Tunamfuatilia (Griezmann) kwa undani kabisa. Amezivutia klabu nyingine pia, lakini tunamfuatilia,". +4 Kipaji maalum: Antoine Griezmann anazivutia klabu kadhaa duniani baada ya kazi yake nzuri akiwa Real Sociedad Lakini pia kuna uwezekano wa Fabregas kurejea Arsenal, mambo ambalo litawafurahisha mashabiki wa timu hiyo. Mustakabali wa kiungo huyo uko shakani kufuatia kuwasili kwa kocha mpya Barcelona, Luis Enrique jambo ambalo The Gunners wamelibaini. Na mabingwa hao wa Kombe la FA hawaoni sababu ya kumfungia milango ya kurejea nyumbani Fabregas, ambaye bado ana uhusiano wa karibu na kocha Wenger. Arsenal ilipewa nafasi ya kwanza ya kumsajili Fabregas wakati inamuuza Barcelona mwaka 2011 iwapo klabu hiyo ya Katalunya itafikiria kumuuza. +4 Yuko njiani kurejea: Arsene Wenger atamrejesha Fabregas msimu ujao?