TUJIKUMBUSHE: MAGOLI YOTE YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA LILILOPITA[2010] NCHINI AFRIKA KUSINI
Pichani
ni Iniesta akifunga goli pekee la Spain katika fainali dhidi ya
Uholanzi. 1-0 ilitosha kuipa Spain ubingwa ambao inaenda kuutetea huko
Brazil.
Mfalme wa soka duniani,Pele, aliwahi kutoa msemo ambao umesimama kwa
miaka nenda rudi.Pele alisema mpira ni magoli.Pigeni chenga na pasi
nyingi weee,lakini mwisho wa siku kitu muhimu kupita vyote ni
magoli.Magoli ndio ushindi.Kitakachoamua bingwa wa Kombe la Dunia mwaka
huu 2014 nchini Brazil ni magoli. Kiatu cha dhahabu[Golden Boot]
kilienda kwa Thomas Muller wa Ujerumani ambaye alifunga magoli 5 katika fainali hizo akiwa amefungana kwa idadi hiyo hiyo ya magoli na Diego Forlan wa Uruguay,Wesley Sneijder wa Uholanzi na David Villa wa Spain.Kabla hatujaanza kushuhudia mabao yakipachikwa na walinda milango wakielekea kwenye nyavu zao kuokota mipira huko nchini Brazil,hebu tujikumbushe ilikuwaje kule nchini Afrika Kusini ambapo bara la Afrika lilipewa nafasi ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. Jumla ya magoli 145 yaliwekwa wavuni.Haya hapa