Profesa Msolla katika moja ya mikutano yake aliyofanya jana jimboni kwake Kilolo, hapa alikuwa kijiji cha Kidabaga Nyomi ya Kidabaga Nyomi ya kijiji cha Lusinga hapa ni kijijini Ndengisivili MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Profesa Peter Msolla amewatoa hofu watanzania akiwahakikishia kwamba chama hicho kitawaletea mgombea urais atakayekata kiu yao. Pamoja na ahadi hiyo, Profesa Msolla ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kilolo amesisitiza kuwania tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 ili akamilishe ndoto za maendeleo alizonazo kwa wananchi wa jimbo hilo. Katika mikutano yake mitatu tofauti aliyofanya juzi katika kata ya Dabaga jimboni humo alisema; “mtasikia mengi kuhusu wagombea urais, lakini niwahakikishieni, CCM ina utaratibu mzuri wa kumpata mgombea wake na ndio utakaotumika katika mchakato wake wa 2015.” “Lakini pia watakuja wengi kwenye majimbo yenye wabunge wa CCM, watakuja na fedha na kuwarubuni; msikubali kurudishwa nyuma kwasababu tunaendelea kusonga mbele, angalieni tuliyofanya na waulizeni wanaokuja wanataka kufanya nini cha ziada ambacho hatuwezi kukifanya,” alisema. Profesa Msolla ni mbunge pekee mkoani Iringa mwenye utaratibu wa kila mwaka wa kutembelea vijiji vyote 106 vya jimbo lake kwa lengo la kuhamasisha na kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuchukua kero mbalimbali za wananchi wake ili zifanyiwe kazi na mamlaka zinazohusika. “Kama kawaida yake chama kitawaletea mgombea mwenye viwango, anayekubalika, mwenye maono, mchapakazi atakayedumisha amani ya nchi na atakayehakikisha Ilani ijayo ya CCM inasimamiwa ipasavyo,” alisema. Akiwa katika vijiji vya Lusinga, Ndengisivili na Kidanaga, Profesa Msolla alisema wana CCM na wafuasi wake wote wanapaswa kushiriki ipasavyo katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kwa kuwa ni muhimu katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. “Ili tuunde serikali imara, itakayoendeleza mazuri yote tunayoendelea kuyafanya ni lazima tupate ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,” alisema. Aliwataka watanzania kuwapuuza wanasiasia wanaohamasisha vurugu huku akidokeza kwamba hali hiyo ikishika hatamu hakuna atakayekuwa salama na athari kubwa zaidi zitakuwa kwa watoto, wanawake na wazee. “Sisi wenyewe ndio walinzi wa amani tuliyonayo; tukiwakaribisha wanaotaka kuivuruga hakika waliomo katika vurugu na wasiomo wataathirika,” alisema. Kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya Alisema wanaong’ang’ania muundo wa serikali tatu hawaitakii mema nchi hii na baadhi yao ni wale wanaotoka katika kundi linalotaka kuhatarisha amani ya nchi. Alisema muundo wa serikali ni jambo kubwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kwa lengo la kudumisha maelewano na amani baina ya pande mbili za muungano, muundo wa sasa wa serikali mbili ndio muafaka. Profesa Msolla alisema muundo wasasa wa muungano ndio muundo unaoshughulikia maendeleo ya watu kwahiyo unapaswa kudumishwa. “Tunasababu gani ya kuwa na serikali ya tatu isiyowajibika moja kwa moja kwenye majukumu muhimu ya wananchi kama kilimo, afya, biashara, miundombinu, elimu na mengineyo?” alisema. Serikali ya tatu inayopigiwa debe na baadhi ya wanasiasa itakuwa tegemezi na kwasababu hiyo itaongeza mzigo kwa wananchi. Aliwataka wananchi wa jimbo lake kujitokeza kwa wingi kuunga mkono maazimio yatakayofikiwa na wajumbe wa bunge la katiba kuhusu katiba wanayoitaka. “Tukishakamilishamchakato katika bunge hilo, rasimu hiyo italetwa kwa wananchi ili ipigiwe kurana itakapoungwa mkono, nchi itakuwa imepata katiba mpya,” alisema