Muigizaji mkongwe Chausiku Salum ‘Bi Chau’. Akipiga stori na paparazi hivi karibuni, Bi. Chau alisema amekuwa akipokea simu nyingi zikimuuliza anakalia wapi eda ili wakampe pole huku wengine wakihoji kwa nini atembea mtaani wakati amefiwa. Marehemu mzee Small akiwa na Bi Chau enzi za uhai wake. Muigizaji mkongwe Chausiku Salum ‘Bi Chau’ ameshangazwa na dhana iliyopo kwa mashibiki kwamba yeye ni mke wa marehemu Saidi Ngamba ‘Mzee Small’ huku wakimtaka akae eda. “Baada ya mazishi nilipata wakati mgumu, nilipokuwa nikienda kazini ITV nilichukua Bajaj lakini nilipokelewa na maneno makali ambapo niliambiwa sisi wasanii ni wabaya sana, nimeona kafariki hata siku hazijaisha nimepaka piko na sijakaa eda, nilijisikia vibaya kwani Small hakuwahi kuwa mpenzi wangu,” alisema Bi. Chau.