SASA UKAWA yatoa tathmini ya ziara zake
WANANCHI wengi nchini wamejitokeza kutaka Bunge la Katiba lijadili
rasimu ya pili iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba na siyo nyingine.
Msimamo huo wa wananchi umo kwenye tathmini iliyofanywa na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ilipozunguka kwa siku 14 nchini kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa katiba.
Ziara hiyo ilikuwa na timu tatu zilizogawanywa kwa kanda ambapo Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambari (Kanda ya Kati), Katibu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa (Kanda ya Kaskazini) na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba (Kanda ya Nyanda za Juu Kusini).
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Dk. Slaa alisema akiwa katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, wananchi bila kujali itikadi za vyama na dini zao, walionyesha kukerwa na wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokuwa tayari kujadili rasimu ya Jaji Warioba.
“Tuliulizwa maswali mengi ya kutaka ufafanuzi kwanini wajumbe walikuwa wakijadili maoni yao badala ya maoni ya wananchi… tuliwaeleza bila kuficha kuwa CCM ilikuwa na rasimu waliyotaka ipite, ndiyo maana UKAWA waliamua kutoka nje,” alisema.
Dk. Slaa alisema katika ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu mchakato huo, wananchi wengi walionyesha kukerwa na hatua hiyo ya CCM kuteka mjadala na kutaka wajumbe wa UKAWA wasirejee bungeni hadi hapo watakapohakikishiwa kuwa rasimu ya Jaji Warioba ndiyo itakayowasilishwa.