Wakati Ghana inajiandaa kukabiliana na Marekani leo katika Kombe la Dunia, mcheza filamu maarufu wa Ghana Nikki Samonas amesema atampa busu zito mchezaji yeyote wa Ghana atakayefunga bao la kwanza hii leo. Kwa mujibu wa Nikki, busu hilo litakuwa zito na tamu kwa sababu yeye ni 'mbusuji' mzuri na hiyo ni ahadi ametoa. Amesema kwa kuwa hayupo Brazil kwa sasa busu hilo litatolewa wakati wachezaji wa Black Stars watakaporejea. Taarifa na picha kwa hisani ya Showbiz News.(A.I)