Header Ads

Mrema awatambia Ukawa, amwonya Mbatia

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) amedai kitendo cha yeye kubaki kwenye Bunge Maalumu la Katiba kumetumiwa vibaya na wahasimu wake wa kisiasa jimboni kwake.
“Ukawa na ubunge wa Vunjo vimegeuka propaganda chafu dhidi yangu. Wamediriki kuwaambia wananchi wangu kuwa nimeahidi kuwaachia jimbo langu,” alisema.
Mrema ambaye pia ni mwenyekiti wa taifa wa TLP, alitoa kauli hiyo jana jimboni kwake katika mkutano na waandishi wa habari aliouitisha kuelezea kwa nini hakuwaunga mkono Ukawa.
Mrema alisema malengo ya Ukawa siyo katiba bali Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na ndiyo maana tangu waliposusia Bunge agenda yao imebadilika na kuwa muungano wa kuelekea uchaguzi 2015.
“Mimi nimeamua kubaki bungeni kwa ajili ya masilahi mapana ya wananchi wa jimbo langu la Vunjo na Watanzania kwa jumla. Sitishwi na Ukawa na nitatetea kiti changu 2015,” alisisitiza.
Mrema alitumia mkutano huo kumshambulia mbunge wa kuteuliwa na Rais, ambaye ni James Mbatia kutokana na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo mwakani. Kwa mujibu wa Mrema, ndiye Mtanzania pekee mwenye sifa na aliweza kugombea ubunge katika majimbo matatu tofauti na kushinda.
“Mimi ni Mtanzania pekee ambaye nimewahi kuwa mbunge wa majimbo matatu tofauti ya Moshi Vijijini, Temeke na Vunjo. Sifa hizo hazipo kwa wengine,” alisema.
Powered by Blogger.