Ndege nyingine yaanguka na kuua abiria wote
Ndege ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makazi ya watu baada kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Magharibi mwa mji wa Tehran nchini Iran.
Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kwa teknologia ya Ukraine imepata ajari na kuua watu wote waliokuwepo kwenye hiyo ndege.
Kituo cha television cha taifa kimetangaza kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 40 na uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.
Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza