WAUMINI WA KANISA LA ANGLIKANA NYAMAGANA WALETA VURUGU KANISANI
Waumini
wa kanisa la Anglikana Wilaya ya Nyamagana Mwanza walisimamisha kwa
muda shughuli za ibada kanisani hapo baada ya kutokea vurugu kubwa.
Vurugu
hizo zilitokea baada ya baadhi ya waumini hao kumtuhumu Askofu wa
kanisa hilo Boniface Kwangu kwamba ni mmoja wa wafuasi wa kundi la
Freemasons na hufanya kazi za kundi hilo.
Mmoja wa waumini wa kanisa hilo Shadrack Lazaro alitoa
tamko
la jinsi askofu wao anavyofanya kazi na kundi la Freemason ndipo
waumini walipomvamia na kumtoa nje ya kanisa kwa nguvu na kusababisha
vurugu kubwa.
Muumini
huyo alisema pamoja na sababu kadhaa za kumkataa askofu huyo pia
hawaridhishwi na tabia yake ikiwemo kutaka kubomoa sakafu akidai kuna
irizi imefichwa na baadhi ya waumini wake kanisani hapo