SARAH K KUTIKISA NDANI YA JIJI LA ARUSHA NA KIBAO CHAKE KIPYA KABISAAA!!!
Katika hali inayotaswiriwa kuwa wakazi wa Jiji la Arusha na viunga vyake wana bahati kubwa sana kwa kuwashuhudia waimbaji wa nyimbo za Injili wakiwa katika jiji hilo Msanii wa Afrika Mashariki SARAH K atapata fursa ya kukitambulisha kibao chake kipya ndani ya tamasha la Upendo kwa mama.
Sara K ambaye amekuwa akitamba na vibao mbalimbali vya Injili na ambaye ametikisa sana na kuwa na mashabiki wengi katika nchi za Afrika Mashariki na Kati atatambulisha kibao chake kipya kabisa siku ya tarehe 02/11/2014 katika tamasha hilo litakalofanyika katika Uwanja wa SHEKH AMRI ABED jijini Arusha.
Kwa upande wake Sarah K amesema kuwa amejipanga kikamilifu kuweza kutoa burudani kabambe kwa wakazi wote wa Arusha pamoja na watu wenginge watakao hudhuria katika Tamasha hilo kubwa ambalo halijawahi kufanyika ndani ya Jiji hilo na Hapa Tanzania.
Amesema atakuja na kikosi kilicho kamilika ili kuonyesha upendo kwa MAMA pamoja na kuonyesha Upendo kwa wakazi na mashabiki wote sambamba na kukitambulisha kibao hicho tena kwa mara ya kwanza.
Wasanii watakao hudumu katika Tamasha hilo ni pamoja na UPENDO NKONE,MARTHA MWAIPAJA,CHRISTINA SHUSHO,ENG CARLOS MKUNDI,BARAKA MASSA,FLORA MWENDA,ESTER BUKUKU,MESS CHENGULA,pamoja na wasanii mbalimbali.