Header Ads

TAMASHA LA INJILI LA UPENDO KWA MAMA LAWA GUMZO WAKAZI MKOANI ARUSHA.

 




Wananchi wa Mkoani Arusha wamefurahishwa na ujio wa wasanii maarufu Afrika Mashariki na Kati wa nyimbo za Injili katika Tamasha lijulikanalo UPENDO KWA MAMA na kusema kuwa Tamasha hilo litakuwa la kihistoria kwani lina manufaa makubwa kwa wakina MAMA.


Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti Wananchi hao wamesema kuwa wanapenda kushuhudia wasanii hao ambao wanawatazama kupitia Luninga na hivyo itakuwa n fursa kwao kuwatazama live.

Wamedai kuwa licha ya kuwatazama wasanii hao ambao nia UPENDO NKONE,CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA,SARAH K ambaye atatambulisha kibao chake kipya siku ya tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02/11/2014.katika uwanja wa SHEKH AMRI ABED Jijini Arusha.

Waimbaji wengine watakao hudumu siku hiyo ikiwa ni pamoja na kuwaombea watu mbalimbali wenye shida na matatizo sambamba na kutoa misaada ya mitaji kwa wakina mama ni pamoja na Eng CARLOS MKUINDI,MASSA BARAKA,FLORA MWENDA,ESTER BUKUKU,MESS CHENGULA,NESTA SANGA MAMA WA CHAGUO LAKO PAMOJA NA MATUMAINI.


Powered by Blogger.