MADIWANI CCM, CUF WAKUNJANA, KIKAO CHASAMBARATIKA
Kikao
cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga, kimevunjika
mara tatu mfululizo kutokana na madiwani wa Chama cha Wananchi (CUF) na
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanyiana vurugu na kukunjana kutaka
kuzichapa kavu kavu.
Vurugu hizo zilianza saa 3:00 asubuhi baada ya Meya wa Jiji hilo, Omar Gulled, kufungua kikao hicho.