Mahakama kuu Zanzibar yakanusha taarifa ya Mwanahalisi
Mahakama kuu ya Zanzibar
imekanusha vikali taarifa iliotolewa na Gazeti la mwanahalisi linalochapishwa
kila wiki nchini iliodai kuwa Mahakama kuu Zanzibar inampango wa kuandaa
mazingira ya kuwatumia wanasheria wakujitegemea kuweza kufunguwa kesi
zinazohusu masuala ya uchaguzi kwa Makamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na
wahusika wengine.
Imeelezwa taarifa hizo zinazodai
mahakama inatumika ni za uchochezi na
kutaka kushusha hadhi ya mahakama.
Pamoja na mambo mengine wametowa
siku saba kwa Gazeti hilo kuomba Radhi vinginevyo Mahakama itaangalia namna ya
kufuata taratibu za kisheria dhidi ya gazeti hilo.
Akizungumza na wanahabari
Ofisini kwake mahakama kuu Zanzibar Mrajisi wa mahakama kuu joge
Kazi anasema ameshangazwa na taarifa ya
gazeti hilo ambalo amedai limeshidwa hata kufanya utafiti wa kufika ofisi za
mahakama ili kujiridhisha na hali hiyo.
Aidha Joge Kazi anasema taratibu
za kimahakama sio kutafuta kesi bali ni kupokea kesi kutoka kwa mkurugenzi wa
mashtaka na wala sio mahakama kuu na kulitaka gazwti hilo
kuacha kuandika taarifa za kichochezi hasa katika kipindi hiki cha mpito kwa
Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine Joge kazi
anawataka waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi zao waache kuchochea
na kukubali kutumiwa kisiasa hali ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani
nchini.