Wananchama wa CUF wafungua kesi kupinga matokeo Ubunge Tabora Mjini
Wanachama wa Chama cha wananchi
CUF Wilaya ya Tabora wameamua kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tabora kupinga
matokeo ya Ubunge wa jimbo la Tabora Mjini yaliyompa ushindi mgombea wa CCM
Emmanuel Mwakasaka.
Wanachama hao wamesema wameamua
kufungua kesi hiyo kwa vile wana amini ushindi wa Mgombea wa CCM haukuwa halali
na wanataka utengeuliwe.
Mahakama inazidi kuaminiwa na
wananchi ambao wanafungua shauri kupinga ushindi wa mgombea wa Chama cha
Mapinduzi,Emmanuel Mwakasaka na kuungwa mkono na aliyekuwa mgombea wa Chama cha
wananchi CUF.
Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya
uchaguzi mkuu ni ya tatu kufunguliwa katika Mahakama Kuu kanda ya Tabora.