Viongozi wa Chadema Mtwara waulalamikia uongozi wa Taifa Uteuzi Viti Maalum
Viongozi wa Mkoa na Wilaya wa Chama cha Demokrasia na mendeleo CHADEMA
Mkoani Mtwara wamelalamikia uongozi wa
Taifa katika uteuzi wa nafasi za Ubunge pamoja Udiwani Viti maalumu Bila ya
kushirikishwa hali iliyosababisha kuteuliwa viongozi tofauti na
waliopendekezwa.
Hii imetokana na kuapishwa kwa
Diwani Lulu Ngachinja ambaye hawakumpendekeza katika vikao Rasmi vya Wilaya na Mkoa.
Katibu mwenezi wa Wilaya Hamis Bakari ametishia
kuachana na chama hicho kutokana na kushindwa kuelewa taratibu zinazitumika
katika uteuzi wa wabunge pamoja na madiwani wa viti maalum ambao tayari
wamekwisha apishwa tayar kwa kuanza kazi.
Wakiongea katika ofisi za mkoa
Mtwara baadhi ya viongozi pamoja na aliyekuwa mgombea Udiwani viti maalum
wanasema uteuzi huo umekuja tofauti na walivyopanga katika vikao
na kuamua nani Wa kuwawakilisha katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Hamis Bakar katibu mwenezi wa
Wlaya mtwara anasema nafasi ya Mbunge Viti maalumu imepewa mtu ambaye
hawakuwahi kufanya naye kazi katika kipindi chote cha Kampeni.
Baadhi ya maeneo wameendelea
kutoa malalamiko juu ya uteuzi wa viti maalum kwa wabunge na madiwani jambo
ambalo uongozi wa Chadema Taifa wanapaswa kulitolea Ufafanuzi.