Wauguzi Z’bar wahimizwa kufuata misingi ya taaluma
Katika kuhakikisha jamii
inapatiwa huduma bora hususani za afya wanafunzi wa chuo cha sayansi ya
afya Mbweni kilichopo visiwani Zanzibar wametakiwa kutekeleza
majukumu yao ipasavyo ili kuihudumia jamii kwa kufuata
misingi ya taaluma zao.
Hali hiyo itasaidia
kupunguza malalamiko kwa wagonjwa ambao kwa kiasi
kikubwa kada ya uuguzi ndiyo
inayolalamikiwa kutokana na baadhi ya
wahudumu wa afya kutoa lugha chafu pale
wanapowahudumia wagonjwa.
Baadhi ya kazi
zilizoonyeshwa na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa
ni mafunzo wanayofundishwa ni kwa jinsi
gani watatoa huduma kwa wagonjwa pale wanapofika
katika vituo vya afya kutokana na ugonjwa husika , ikiwa ni maonyesho ya
tano ya umoja wa wanafunzi wa chuo hicho yanayofanyika
kila mwaka chuoni hapo.
Licha ya kuonyesha kazi
hizo Mkurugenzi wa Utumishi na Rasilimali Watu kutoka
wizara ya afya omary mwinyinkondo anasema itakuwa vyema basi
yale waliyoyafanya chuoni haapo yakataekelezwa hata pale wanapopata
nafasi yakuwahudumia wagonjwa , kwa kuwa imebainika kuwa
wafanyakazi wengi pale wanapopata mikataba maadili
wanayaacha vyuoni na kushindwa kutekeleza sehemu za kazi na
kuondosha imani kwa wagonjwa.
Akizungumza kwa niaba
ya wanafunzi , rais wa chuo hicho sleiyoum abdallah ali anasema
kuwa licha ya kuonyesha kazi hizo bado wanakabiliwa na changamoto nyingi
ya vitendea kazi .
walimu wakisisistiza maadili hayo
kwa wanafunzi basi malalamiko yatapungua sehemu za kazi
sanjari na watumishi wenyewe wakiwa tayari kufuata missing
hiyo ikiwa ni maoni ya baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.
Sula la kufuata maadili katika
utendaji kazi ni ya kila kada hivyo ni wajibu
kutekeleza maadili hayo kivitendo ili kuepuka mawazo
hasi kwa wanajamii kuhusu kada husika.