Mahakama yawaruhusu wasichana wavae hijab wawapo shuleni
Mahakama ya Rufaa nchini Kenye imesema kuwa Wasichana wa kiislam wanaosoma shule wanapaswa kuruhusiwa kuvaa hijab kama sehemu ya sare za shule .
Uamuzi huo wa kihistoria uliotolewa na majaji watatu umekuja baada ya kanisa la kimethodist kupinga muongozo kutoka kwa mamlaka za nchi hiyo kuwaruhusu wasichana wa shule wa kiislamu kuvaa hijab ama vilemba katika shule yake.
Wanafunzi wa kiislam katika shule ya sekondari ya St Paul Kiwanjani School kaunti ya Isiolo walipigwa marufuku kuvaa hijab na suruari nyeupe pamoja na sare ya shule.
Kanisa hilo lilidai kuwa uamuzi wa kuwaruhusu wanafunzi wasichana wa kiislamu kuvaa mavazi tofauti umesababisha uhasama miongoni mwa wanafunzi.
Mahakama ya juu iliunga mkono kanisa na kusema kuwa wasichana hawawezi kuvaa hijkabu shuleni.
Lakini majaji katika mahakama ya rufaa wamesema kuwa ni jukumu la wanaotoa elimu kukubali maadili na kanuni za utu, na za matabaka mbali mbali ya watu, na bila ubaguzi , limeripoti gazeti la Star nchini Kenya.
Kwa mujibu wa gazeti la East African Standard, majaji hao waliongeza kusema kuwa vazi la kidini haliwezi kulinganishwa na mtindo wa vazi unaokwenda na wakati
Shule za kitaifa huruhusu wasichana kuvaa hijab.