Header Ads

Je wajua Twiga wote hawafanani?

Utafiti wa jeni za twiga umebaini kwamba kinyume na ilivyodhaniwa awali, kwamba twiga wote ni wa jamii moja imebainika kuna jamii nne tofauti za twiga.

Uchunguzi wa chembe za msambojeni (DNA) za twiga wanaoishi nchini Namibia umegundua kuna aina nne tofauti za twiga na twiga hao hawajajamiiana kwa mamilioni ya miaka.
Wanasayansi wametaja makundi hayo kuwa twiga wa kusini, twiga wa kaskazini, twiga wa Kimaasai na twiga 'reticulated'.
Wakfu wa Uhifadhi wa Twiga, uliofadhili utafiti huo, umesema matokeo ya utafiti huo yatasaidia katika juhudi za kuwalinda na kuwahifadhi wanyama hao na mazingira yao.
Aina ya twiga:
  • Twiga wa kusini (Giraffa giraffa)
  • Twiga wa Kimaasai (G. tippelskirchi),
  • twiga 'reticulated' (G. reticulata)
  • twiga wa kaskazini (G. camelopardalis), ambao wanajumuisha twiga wa Kinubi (G. c. camelopardalis) ambao ni jamii ndogo.
Kila aina ya twiga imezoea mazingira na ina tabia tofauti.
Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, idadi ya twiga duniani imepungua kwa 40% - na sasa inakadiriwa kwamba kuna twiga 90,000 porini.
Kwa pamoja, wanachukuliwa kama wanyama wasio hatarini ya kuangamia lakini wanasayansi sasa wanasema kwa kuangazia kila aina, huenda tofauti ikabainika miongoni mwa idadi ya kila aina ya twiga.
Ni vyema kuhamaisha watu kuhusu uhifadhi wa twiga, "wanyama maridadi ambao bado hatufahamu mengi kuwahusu," anasema Axel Janke, mtaalamu wa jeni kituo cha Senckenberg, ambaye aliongoza utafiti huo.
BBC
Powered by Blogger.