CLARENCE SEEDORF MENEJA MPYA AC MILAN
MCHEZAJI VETERANI kutoka Netherlands, Clarence Seedorf, anatarajiwa kuwa Meneja mpya wa AC Milan ya Italy baada kutangaza kustaafu kucheza Soka.
Seedorf, Miaka 37, ambae aliichezea
Klabu hiyo Kigogo ya Italy kati ya Mwaka 2002 hadi 2012, anambadili
Massimiliano Allegri alietimuliwa kazi Jumatatu.
.....................................................................................
Clarence Seedorf:
-Umri: Miaka 37
-Uraia: Netherlands
-Klabu: Ajax (1992-95); Sampdoria (1995-96); Real Madrid (1996-2000); Inter Milan (2000-02); AC Milan (2002-2012); Botafogo (2012-2014)
-Holland: Mechi 87
Msimu huu, kwenye Serie A, AC Milan wanasuasua kwa kushinda Mechi 5 tu kati ya 19 na wako Pointi 30 nyuma ya Vinara Juventus.
Jumapili iliyopita, AC Milan ilichapwa Bao 4-3 na Sassuolo.
Akiwa na AC Milan, Seedorf alicheza Mechi zaidi ya 400 na kutwaa Ubingwa wa Serie A mara 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 2.
Pia, Seedorf alikuwa Mchezaji wa Kwanza
kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI mara 3 na Klabu 3 tofauti baada kushinda
akiwa na Ajax Mwaka 1995, Real Madrid 1998 na AC Milan, Miaka ya 2003 na
2007.
Seedorf, ambae pia alizichezea Klabu za
Inter Milan na Sampdoria, baada kuondoka AC Milan alijiunga na Klabu ya
Brazil, Botafogo, Mwaka 2012.