BARCA YABURUZWA KORTINI KUKWEPA KODI UHAMISHO WA NEYMAR!!
BARCA YADAI HAINA KOSA!
Barcelona
imefunguliwa Mashitaka kwenye Mahakama ya Spain kwa udanganyifu kuhusu
ulipaji Kodi unaohusiana na kumnunua Neymar kutoka Santos ya Brazil.
Msemaji wa Mahakama alisema kuwa Jaji Pablo Ruz ameishitaki Barcelona kwa kukiuka Sheria za Kodi kuhusiana na kumnunua Neymar.
Barcelona imekanusha kufanya kosa lolote na imeahidi kutuma Wanasheria wake Mahakamani ili kujisafisha.
Pamoja na Kesi hii, pia Mahakama chini
ya Jaji huyo huyo inachunguza malalamiko ya Mwanachama wa Barcelona,
Jordi Cases, ambae ameungwa mkono na Waendesha Mashitaka wa Spain
waliokubaliana na Madai yake kwamba kulikuwepo na ubadhirifu na
ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki wakati wa Uhamisho wa
Neymar.
Kesi hii ilisababisha Rais wa Barca,
Sandro Rosell, ajiuzulu na nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Msaidizi
wake Josep Bartomeu ambae alikiri Uhamisho wa Neymar uligharimu Euro
Milioni 86.2 na sio Euro Milioni 57.1 kama ilivyotangazwa awali.
Mbali ya Kesi kufukuta huko Spain hata
huko Brazil kuna tishio kubwa kwa Barca na upande wa Neymar na Wakala
wake, ambae ni Baba yake Mzazi, kuburuzwa Mahakamani kwa kutowapa Mgao
Wamiliki wengine wa Haki za Neymar ikiwemo Kampuni moja kubwa
inayomiliki Maduka Makubwa huko Brazil
PATA KIINI TAARIFA ZETU ZA AWALI:
+++++++++++++++++
KANDALI UHAMISHO WA NEYMAR: PATA DILI KAMILI!!
Friday, 24 January 2014 09:53
>>RAIS WA BARCA ROSELL AJIUZULU KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU!!
>>KESI IPO MAHAKAMANI!
TAYARI Rais wa Barcelona Sandro Rosell
amejiuzulu na Barcelona imetinga Mahakamani wakichunguzwa kwa Ubadhirifu
wa Fedha kwenye Uhamisho wa Supastaa wa Brazil Neymar kutoka Santos
kwenda Barca mwanzoni mwa Msimu.
Barca wanadaiwa kumnunua Neymar kwa Dau
la Euro Milioni 57.1 lakini ni Euro Milioni 17.1 tu ndizo zilifika
mikononi mwa Klabu yake Santos ya Brazil huku nyingne zote zikikombwa na
Wamiliki wengine waliokuwa na haki nae.
Lakini baadhi ya Wamiliki hao wameibuka
na kudai hawakupata mgao wowote wakiwemo Wamiliki wa Maduka Makubwa,
DIS, huku Kampuni ya N&N, inayomilikiwa na Baba yake Neymar
ikisemekana imekomba Euro Milioni 40.
Hivi sasa, Kesi ipo Mahakamani kwenye
hatua za awali za uchunguzi, na itasikilizwa na Jaji Pablo Ruz, ambae
anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na Barcelona kabla
hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa Ushahidi.
Kesi hii inafuatia malamiko ya
Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ameungwa mkono na Waendesha
Mashitaka wa Spain waliokubaliana na Madai yake kwamba kulikuwepo
ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki.
NINI CHANZO CHA KESI?
Jordi Cases, Mwanachama wa Barcelona,
alifungua Kesi Mahakamani akidai Ubadhirifu wa Fedha na kutokuwepo uwazi
kwenye Uhamisho wa Neymar.
Cases amedai asingefungua Kesi hiyo kama uongozi wa Barca ungemjibu kistaarabu alipohoji undani wa Uhamisho wa Neymar.
NINI KINACHUNGUZWA??
Barcelona, Neymar na Kampuni ya N&N
ilisaini Mkataba Mjini Sao Paulo, Brazil Mwaka 2011 wa Neymar kuhamia
Barcelona Mwaka 2014.
Mkataba huo uliposainiwa, upande wa
Neymar ulipokea Malipo ya Euro Milioni 10 kama Mkopo ambao ungelipwa
baada Neymar kuhamia Barca.
Pia uliweka Dau la Euro Milioni 40 kama haki za Neymar na pia Adhabu ya Euro Milioni 40 ikiwa Makataba huu utakiukwa.
Lakini Mwaka Jana, Santos na Barca,
zilikubaliana Neymar ahame Mwaka mmoja kabla ya makubaliano ya awali na
hivyo Barca kulazimika kulipa Adhabu ya Euro Milioni 40 ikiwa Makataba
huu utakiukwa.
Hilo ndio limeibua wasiwasi kwenye Mamlaka za Spain baada Shabiki Jordi Cases kulalamika.
NINI ANATUHUMIWA ROSELL??
Rosell anatuhumiwa ubadhirifu wa Fedha ambao huko Spain Adhabu yake ni Kifungo kuanzia Mwaka mmoja hadi nane.