KIPIGO CHELSEA KIMEKUJA MASAA 24 BAADA MOURINHO KUMBATIZA WENGER: ‘BINGWA WA KUFELI!’
>>‘MAN CITY WALICHEZA VIZURI KUPITA SISI!!’
>>KIPIGO CHELSEA KIMEKUJA MASAA 24 BAADA MOURINHO KUMBATIZA WENGER: ‘BINGWA WA KUFELI!’
BOSI
wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza Chelsea haikufeli kwa kutupwa nje
ya FA CUP baada ya kuchapwa Bao 2-0 na Manchester City hapo Jana huko
Etihad.
Kipigo hicho cha Chelsea na kubwagwa nje
ya FA CUP kimekuja Masaa 24 tu tangu ambandike Jina Meneja wa Arsenal,
Arsene Wenger, kwamba ni ‘Bingwa wa Kufeli!’
Madai hayo ya Mourinho yalifuatia kauli
ya Wenger kuwa Mourinho anajitoa nafasi ya kuchukua Ubingwa ili akiukosa
asipate lawama na Mourinho kujibu kwa kumkumbusha Wenger kuwa hajatwaa
Kikombe tangu 2005.
Lakini mwenyewe Mourinho ameng’ang’ania:
“Siwezi kusema Timu imefeli. Nitasema City walicheza vyema kupita sisi
na walistahili kushinda!”
Ingawa Chelsea Msimu huu imeifunga Man
City mara mbili kwenye Ligi, mara ya mwisho ikiwa 1-0 Uwanjani Etihad
hapo Februari 3 na kuvunja rekodi ya City ya kutofungwa Nyumbani Msimu
huu, kipigo cha Jana kimeifanya Chelsea itupwe nje na City kutinga Robo
Fainali ya FA CUP.
Hapo Jana Bao za City zilifungwa na Stevan Jovetic na Samir Nasri lakini Mourinho amedai Bao la Nasri lilikuwa Ofsaidi.
Mourinho alisema: “Wao walikuwa Timu
Bora. Wiki mbili zilizopita Timu Bora ilishinda lakini safari hii Timu
Bora imeshinda. Lakini Bao lao la Pili ni Ofsaidi lakini wangeweza
kushinda hata 1-0 kwani hatukukaribia kufunga Goli!”