NAIBU MEYA WA JIJI LA ARUSHA ADAIWA KUTAFUNA ZAIDI YA SHILINGI MILION 8 ZA MRADI WA KISIMA.
Naibu Meya wa jiji la Arusha Bw Prosper Msuya ambaye pia ni diwani wa kata ya Daraja mbili
Unga ltd anadaiwa kutafuna fedha zilizotolewa na manispaa kwa ajili ya kuchimba
kisima cha maji katika mtaa wa Senare kiasi cha zaidi ya shl millioni 8.
Akitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari mjumbe wa serikali ya mtaa wa Senare Bw
Aliamin Msuya amesema kuwa naibu huyo anadaiwa kutumia fedha hizo kwa matumizi
tofauti kinyume na malengo ya fedha hizo kama ilivyotolewa na Almashauri.
Amesema kuwa Naibu huyo fedha hizo ziliombwa kutoka
Almashauri kiasi cha shl million 16 lakini walipewa kiasi hicho cha shl 8
ambacho Msofe alikichukua na kuzitumia kwa matumizi ambayo siyo sahihi na
badala yake aliwapelekea wananchi maji ambayo ni yamsaada kutoka sehemu
ninyinge huku akiwalagai wananchi kuwa ilikuwa ni moja ya ahadi zake.
Bw Msuya amesema kuwa matumizi hayo yasiyo sahihi ni ubadhilifu
wa fedha za serikali kwani katika matumizi ya fedha hizo hakuna kiongozi yeyote
wa mtaa aliyeshirikishwa katika kikao chochote cha kujadili matumizi ya feha
hizo jambo ambalo linaashiria ubadhilifu
na fedha za serikali.
Pamoja na hayo amesema katika kikao cha ODC kilichokaa
kilisababisha sinto fahamu baada ya wajumbe kuhitaji kujua juu wa kuwepo kwa
fedha hizo lakini haikupatikana muafaka
juu ya matumizi halisi ya matumizi ya fedha hizo.
V iongozi huo wanahoji fedha hizo zilitumika kwa kazi gani
na nikwanini kazi iliyofanyia hazibaishwi kama siyo ubadhilifu hivyo kuomba
kiongozi huyo kujitokeza hadharani kudhibisha matumizi halisi ya fedha hizo na
wananchi wapate kuelewa.
Hata hivyo Naibu Meya huyo bw msofe hakuweza kupatikana
kupitia smu yake ya mkononi ili kuweza kudhibitisha tuhuma hizi lakini bado
tunaendelea kumtauta