WACHIMBAJI WADOGO TUNDURU WATEMBELEA MGODI WA MAST LTD KWA AJILI YA KUJIFUNZA NAMNA BORA YA UCHIMBAJI WA MADINI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Kamishna
Msaidizi wa Madini -Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe
kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua namna ya kuendesha uchimbaji salama wa madini kwa
wachimbaji wadogo mara walipotembelea mgodi wa Minerals Access System Tanzania (MAST). Ziara hiyo ni moja ya
mafunzo ya vitendo kwa wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yanayoendelea
Tunduru mkoani Ruvuma.
Mjiolojia
Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea jinsi
madini ya shaba yanavyoweza kutambuliwa kupitia kipande cha mwamba
alichokishika.
Mmoja
wa wachimbaji wadogo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza swali
kwa mwezeshaji Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw.
Julius Sarota (hayupo pichani)
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (aliyevaa shati jeupe)
akiwaelezea wachimbaji wadogo namna uchorongaji wa miamba unavyofanyika mara
wachimbaji wao walipotembelea mgodi wa Minerals
Access System Tanzania (MAST) uliopo Tunduru, Ruvuma.
Mtaalam
wa kampuni ya MAST akionesha namna ya kuchoronga miamba kwa wachimbaji wadogo (
hawapo pichani).
Mtaalam
kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Jones Mushi akionesha jinsi uunganishaji wa mlipuko wa baruti
unavyofanyika kwa wachimbaji wadogo (hawapo pichani) kwenye machimbo ya mgodi
wa MAST uliopo Tunduru, Ruvuma.