HAFLA FUPI YA UJIO WA MKOMBOZI COMMERCIAL BANK BUKOBA.
Mc
wa Hafra hiyo Bw. Andrew Kagya akiwakaribisha wageni Ukumbini, Ukumbi
wa Hoteli ya Coffee Tree iliyopo Bukoba Mjini, ambayo maandalizi yake
yote yamegharimikiwa na kampuni yetu kupitia kinywaji maridadi cha
Climax na Windhoek.
Waimbaji
wa Hapa Mjini Bukoba, Kapotive Star Singers-Bukoba walikuwa tayari
kutumbuiza kwenye hafra hiyo ambayo lengo kuu la hafla hiyo ni kupata
fursa ya kubadilishana mawazo wakati maswala ya kufungua tawi la benki
la Mkombozi Commercial Bank hapa Bukoba.Bwana
Respicius Didace wa Mabibo Beer wines & Spirits LTD akifunguka, Kwa
niaba ya Kampuni yetu ya Mabibo Beer wine and Spirits, kupitia kinywaji
chake cha kimataifa cha Windhoek Premium Lager 100% Pure African Beer
na kinywaji kisicho na kilevi cha Climax Non Alcoholic Herbal Energy
Welcome Drink, tunawakaribisha sana jioni ya leo kwenye hafla fupi
ambayo ni muhimu sana kwetu wana Bukoba.
Leo
tumebahatika kuwa na Mkurugenzi wa Mkombozi Commercial bank ambae
ataweza kutumegea machache kuhusu benki hii, na pia hata sisi tutapata
nafasi kumuuliza maswali ambayo tunadhani yatasaidia katika kuongeza
uelewa wetu kuhusu benki hii. Pia atatuonesha fursa zinazotokana na
uwepo wa benki hii hapa Bukoba hasa kwa kununua hisa zake.
Kampuni
yetu ya Mabibo Beer & Spirits Ltd inaamini katika kuwaleta watu
pamoja, ndio maana wakati wa maandalizi ya hafla yetu hii, tumeawaalika
wafanyabiashara wanaochipukia, wafanyabiashara wakubwa kwa kadiri ya mji
wetu, viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wawakilishi wa baadhi ya
shule maarufu hapa Bukoba, wawakilishi wa wananchi kwenye kata
(Madiwani) n.k. Hii ni fursa ya kufahamiana na watu mbalimbali katika
nyanja mbalimbali wakati tunaendelea kuburudika na vinywaji vyetu vya
Windhoek, na kwa wale ambao hawatumii kilevi wakifurahia Climax (Non
Alcoholic Energy Drink).
Mr. Nicholas Mokirya-Branch Manager Mwanza Branch nae alikuwepo kwenye hafra hii na hapa alikuwa akitoa neno.Mheshimiwa
mgeni rasmi, Mama Edwina Lupembe, Mkurugenzi wa “Mkombozi Commercial
Bank" akiwamegea machache kuhusu benki hiyo ya Mkombozi
Kulia
ni Fr. Vitus Mrosso nae alikuwa tayari kwenye meza kusikiliza wito huo
kwenye hafra hiyo swala zima likiwa ni kununua Hisa za Mkombozi
commercial Bank ili kuweka akiba binafsi.
Lengo
kuu la hafla hii ni kupata fursa ya kubadilishana mawazo wakati
tunapoelekea kufungua tawi la benki la Mkombozi Commercial Bank hapa
Bukoba.
Askofu
Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba akisalimiana
naWaziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Taswira Ukumbini hapo Coffee Tree Hotel katika hafra hiyo iliyokuwa chini ya ya Uzamini wa Udhamini wa Windhoek and Climax.
Fr. Vitus Mrosso akiuliza swali kuhusu swala zima la Benki hiyo ya Mkombozi na Mikopo yake
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka(kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Edwina Lupembe (kulia) wakifurahia jambo kwenye
meza kuu wakati wa hafra hiyo.
Bi. Edwina
Lupembe hakuishia hapo kujibu maswali tu aliendelea pia kuwapa faida za
benki hiyo ya Mkombozi na kuwataka wakazi wa Bukoba kuendelea kununua
Hisa kwa wingi zaidi.
Askofu
Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia) akitoa
neno, Benki ya Mkombozi ni sauti ya kinabii inayolenga kuwaletea
watanzania ukombozi wa kweli. Benki ya Mkombozi iliyozinduliwa mwaka
2009, kwa kianzio cha mtaji wa Shilingi Bilioni sita nukta nane, mchango
wa waamini wa Kanisa Katoliki, inalenga kuwasaidia watu wa kipato cha
chini kuinua hali yao ya maisha na wawekezaji kupanua kiwango chao cha
kuwekeza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote pasipo na ubaguzi.Askofu
Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba (kulia)
akionesha juu kwa wale ambao hawatumii kilevi wakitumie Climax (Non
Alcoholic Energy Drink). Ambapo maandalizi yote yamegharimikiwa na
kampuni kupitia kinywaji maridadi cha Climax na Windhoek.
Hata
na mimi natumia kinywaji hiki cha Climax (Non Alcoholic Energy
Drink) Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba
akikinanga kinywaji hicho!
Askofu
Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki Bukoba, ni kati ya wajumbe
wa Kikosi kazi, waliopewa dhamana kushughulikia mchakato wa uanzishwaji
wa Benki ya Mkombozi nchini Tanzania. Hii ni sauti ya kinabii, katika
mapambano dhidi ya umaskini. Ninakualika sasa uweze kujiunga na Askofu
Msaidizi Kilaini kwa ufafanuzi zaidi kuhusu dhamana ya Kanisa ndani ya
Jamii na Benki ya Mkombozi.
Picha na habari na Faustine Ruta