MALEJENDARI KUCHEZA MECHI DHIDI YA UMASKINI!
>>Ronaldo, Zidane & Friends vs BSC Young Boys & Friends!!
>>REFA NI LEJENDARI PIERLUIGI COLLINA!!
>>JUMANNE, MACHI 4, BERN, USWISI, SAA 4 USIKU!
MALEJENDARI
wa Soka watashiriki Mechi ya Maonyesho huko Berne, Uswisi Jumanne Usiku
ili kuchangisha Fedha kusaidia Nchi ya Philippines iliyokumbwa na
Tufani Haiyan.
Mechi hiyo itachezwa kati ya Timu ya
Ronaldo, Zidane and Friends dhidi ya Klabu ya Uswisi, BSC Young Boys,
ambayo itashirikisha Nguli wao wengine na kuitwa BSC Young Boys and
Friends kwa ajili ya Mechi hii.
Hii itakuwa Mechi ya 11 ya kila Mwaka
ambayo hutayarishwa mahsusi kupinga Umaskini Duniani na itaitwa ‘11th
Annual Match Against Poverty’.
Miongoni mwa Timu ya Ronaldo, Zidane
and Friends ni Malejendari Ronaldo, Zinedine Zidane, Luis Figo na Paolo
Maldini na Kocha wao atakuwa Ruud Gullit huku Wachezaji wengine wakiwa
kina Fernando Hierro, Fabio Cannavaro, Robert Pires, Patrick Vieira,
Gennaro Gattuso, Pavel Nedved, Christian Vieri na Giovane Elber.
Timu ya BSC Young Boys and Friends
itaongozwa na Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Uswisi Stephane
Chapuisat pamoja na Hakan Yakin.
Refa wa Mechi hii ni Lejendari wa Marefa Pierluigi Collina.
RONALDO, ZIDANE & FRIENDS-WACHEZAJI WALIOTHIBITISHWA:
MAKIPA |
Carlo Cudicini (Italy), Antonios Nikopolidis (Greece) |
MABEKI |
Paolo Maldini, Fabio Cannavaro, Gianluca Zambrotta (Italy),
Fernando Hierro, Michel Salgado (Spain), Jamie Carragher (England),
Paulo Ferreira, Fernando Couto (Portugal) |
VIUNGO |
Zinedine Zidane, Patrick Vieira, Robert Pires, Christian
Kerembeu (France), Luis Figo, Paulo Sousa (Portugal), Pavel Nedved
(Czech Republic), Freddie Ljungberg (Sweden), Gaizka Mendieta (Spain),
Gennaro Gattuso (Italy), Ronald de Boer (Netherlands), Santiago
Solari (Argentina), Hidetoshi Nakata (Japan), Steve McManaman
(England) |
MASTRAIKA |
Ronaldo, Marta, Giovane Elber (Brazil), Davor Suker
(Croatia), Hakan Sukur (Turkey), Youri Djorkaeff (France), Christian
Vieri (Italy), Nuno Gomes (Portugal). |