MAN UNITED: TUMEPATA BONGE LA HASARA KWA KUVURUNDA.
Pamoja na hayo, Woodward
amesema kwamba haitaiathiri k;abu hiyo katika solo la usajili. "Kutokana
na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa Pauni Milioni 30 za
michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni kurejea kwenye Ligi ya
Mabingwa naa utaona kwenye usajili wetu,".
Mazungumzo: Giwji wa United, Ryan Giggs alipigwa picha nchini Uholanzi akiwa na kikao na Van Gaal Jumatano
Akizungumza katika mkutano wa
simu, alisema: "Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza vibaya katika nafasi
tab saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano ya Ulaya.
"Kuwa na uhakika kila mmoja
katika klabu anapambana kuhakikisha msimu ujao tunakuwa katika kiwango
cha juu cha Manchester United.
"Tumefanya mabadiliko ya bench
la Ufundi Aprili, tumefurahi kuwa na Ryan Giggs kwa kumalizia msimu
vizuri. Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kupata kocha mpya na
tarajia atatangazwa muda si mrefu,".
Louis van Gaal ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua Manchester United baada ya Fainali za Kombe la Dunia atakapoiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo na Van Gaal kwa niaba ya klabu