PICHA ZA YULE KIJANA ALIYENG'ATWA ULIMI NA JIMAMA HUKO MKOANI ARUSHA
Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja aliyefahamika kama Mama Abuu
amefanya tukio la ajabu baada ya kumng’ata na kumkata ulimi kijana Paulo
Simon mwenye umri wa miaka 18, kufuatia ‘Serengeti Boy’ huyo kukataa
kufanya naye mapenzi katika eneo la Tindigani, Kimandolu mjini Arusha
hivi karibuni.
Akisimulia kwa kuandika kwenye karatasi, Simon ambaye sasa amelazwa
katika Hospitali ya Mount Meru jijini hapa, alisema alikuwa akiuza baa
katika eneo hilo wakati mwanamke huyo alipotokea na kukaa kaunta na
kuanza kunywa pombe kama wateja wengine.
Alisema ilipofika saa 6:30 usiku wateja wengine wote waliondoka na
kubakia mama huyo pekee, kitu kilichomfanya naye afunge baa. Lakini
alipomaliza kufanya hivyo mama huyo alimfuata na kumweleza kuwa
alihitaji kufanya naye mapenzi.
“Sikuwa na mazoea naye, nilipokataa kufanya naye mapenzi,
alinisogelea na kunishika sehemu zangu za siri na kuanza kuzivuta,
nilipopiga kelele akanishika kichwa na kunilazimisha ‘kunidendesha’,
akafanikiwa kuingiza mdomo wake kwangu na kunikata ulimi wangu,
akaondoka nao na kwenda kuutema karibu na mlango wa bar,” alisema Simon
ambaye wahudumu wa hospitali hiyo wamelazimika kumwekea ndoo ili awe
anatemea damu kutokana na kujaa mdomoni.
Alisema baada ya kukatwa ulimi ambao sasa unamletea maumivu makali,
alifanikiwa kufika nyumbani kwake kabla ya tajiri yake kumchukua na
kumpeleka hospitalini ambako amelazwa.
Jeshi la Polisi mkoani hapa limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa ameshatiwa mbaroni huku uchunguzi ukiwa unaendelea. Hali ya majeruhi inaendelea vizuri.